MSANII wa muziki kutoka Tanzania, Grace Matata ameachia kazi mpya na ya kwanza kwa mwaka huu wa 2020 ikiwa ni wimbo wa kwanza kabisa kusikika kutoka kwenye upcoming EP project ya REBIRTH.
Wimbo unakwenda kwa jina la ‘Me and You’ na ni miongoni mwa nyimbo nne (4) zinazopatikana kwenye EP project ya REBIRTH. Kazi hiyo mpya imefanyika kwenye studio za Fisher Records zilizopo Kunduchi, Dar Es Salaam chini ya Mtayarishaji wa muziki Taz Goemi.